September 11, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mpina ashinda kesi, mahakama yamruhusu kurudisha fomu

Luhaga Mpina, Mgombea Urais wa ACT Wazalendo

 

MGOMBEA Urais wa JMT kupitia ACT Wazalendo, Luhaga Joelson Mpina ameruhusiwa kurudisha Fomu ya Uteuzi na Tume Huru ya Uchaguzi imeamriwa kupokea na kuendelea na taratibu nyinginezo. Anaripoti Mwandishi Wetu. Dodoma … (endelea).

Hayo ni maelekezo ya Mahakama Kuu chini ya jopo la Majaji watatu waliosikiliza shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mpina pamoja na chama chake.

Chama cha ACT Wazalendo na Mpina walifungua shauri kupinga uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi [INEC] wa kumuengua kugombea baada ya kumzuia kurudisha Fomu ya Uteuzi siku ya tarehe 28 iliyokuwa ya mwisho kwa wagombea urais kuwasilisha fomu zao.

Tume inayoongozwa na Jaji Jacobs Mwambegele, ilifikia uamuzi huo kwa maelezo kuwa amekosa sifa kutokana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania iliyoeleza kuwa Mpina aliteuliwa kwa kukiuka katiba na kanuni za chama chake.

Na uamuzi hup wa Msajili ulitokana na malalamiko yaliyowasilishwa na mwanachama na kiongozi wa chama hicho, Monalisa Joseph Ndala aliyedai kuwa mkutano mkuu uliompitisha Mpina haukufuata katiba.

About The Author

error: Content is protected !!