September 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mke wa Rais Ivory Coast ajitosa kwenye mbio za urais

 

MKEWA wa rais wa zamani wa Ivory Coast, Simone Gbagbo (76), amejitosa katika kinyang’anyiro cha urais. Inaripoti Mitandao ya Kimatiafa  … (endelea).

Jina la Simone, limeonekana katika orodha ya wagombea watano walioidhinishwa rasmi kugombea nafasi hiyo, katika uchaguzi wa mwezi ujao. Anatarajiwa kukabiliana na rais  wa sasa, Alassane Ouattara (83), anayetetea wadhifa wake.

Outtara alichukua mamlaka ya urais baada ya kumshinda Laurent Gbagbo – mume wa Simone – aliyekamatwa kwenye chumba cha kulala cha rais wakati wa mzozo ulioikumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa 2010.

Rais huyo wa zamani ameondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho, kama ilivyo kwa aliyekuwa waziri mkuu Pascal Affi N’Guessan na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Credit Suisse Tidjane Thiam.

Kuondolewa kwao kumeibua wasiwasi kuhusu uhalali wa uchaguzi wa 25 Oktoba na kuzua hofu ya kukosekana kwa utulivu.

About The Author

error: Content is protected !!