September 9, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais Mwinyi: Ubunifu wa majengo nguzo muhimu katika jamii

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ally Mwinyi, amesema fani ya ubunifu wa majengo ni miongoni mwa sekta muhimu zinazochangia kuimarisha uchumi unaokua kwa kasi kila siku. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Mwinyi ameyasema hayo tarehe 8 Septemba 2025, Ikulu Zanzibar alipokutana na timu ya wabunifu wa majengo kutoka Taasisi ya Ubunifu wa Majengo ya Afrika Mashariki,wakiongozwa na Rais wa Taasisi hiyo, Mhandisi Mecky Tchawi.

Rais Mwinyi aliihakikishia timu hiyo, kuwa Zanzibar imeanza kuchukua hatua za kuanzisha kitivu cha taaluma ya ubunifu wa majengo katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu,kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi na ongezeko la miradi ya ujenzi katika sekta mbalimbali za maendeleo.Aidha ,alibainisha kuwa Serikali,kwa kushirikiana na taasisi hiyo,itatafuta mbinu muafaka za kufanikisha utekelezaji wa wazo hilo.

Katika mazungumzo hayo, Rais Mwinyi ameridhia ombi la taasisi hiyo la kuwa mlezi wa kwanza mzawa wa Afrika Mashariki tangu kuanzishwa kwake mwaka 1913,na kukabidhiwa cheti maalum pamoja na kitabu cha historia ya taasisi hiyo.

Kwa upande wake, Raisi wa Taasisi, Mhandisi Mecky Tchawi alisema kasi ya ujenzi wa majengo katika nchi yoyote ni kielelezo cha ukuaji wa uchumi wake.

Alisisitiza kuwa Zanzibar inapaswa kuwa na kitivu cha taaluma ya ubunifu wa majengo ili kuandaa wabunifu vijana wenye ujuzi na weledi wa kisasa.

About The Author

error: Content is protected !!