
Aliyekuwa Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina
MGOMBEA Mwenza wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi amemuomba aliyekuwa kada wa chama hicho na mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina arejee kundini na atampokea kwa mikono yote miwili. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Mpina alijiondoa CCM ambako alikuwa mbunge wa Kisesa kwa miaka 20 na kujiunga na ACT-Wazalendo tarehe 5 Agosti 2025, baada ya kuenguliwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge wa jimbo hilo,
Dk Nchimbi alitoa kauli hiyo leo, tarehe 2 Septemba 2025 akiwa katika Jimbo la Kisesa Mkoani Simiyu akiwa kwenye kampeni za kusaka kura za kwenda ikulu katika uchaguzi utakaofanyika mwishoni mwa mwezi ujao.
“Atakayempigia simu Mpina amwambie kaka yake mkubwa alipita hapa na mwambieni asiponipigia kura atakuwa amekosa adabu ya kisukuma kabisa maana nilipopita si aliwaambia kwamba mimi ni kaka yake, mwambieni kaka yako alipita hapa na anakusubiri na akirudi tena anataka urudishe hiyo kadi ya chama chako kipya (ACT-Wazalendo) urudi CCM na mimi nitapokea kadi ya Mpina. Nitafanya hivyo mwenyewe na wala sitamtuma mtu yoyote” amesema.
ZINAZOFANANA
Wenje aibuka, aunga mkono kususia uchaguzi
Mbunge aliyekaa siku 8 ACT-Wazalendo arudi CCM
Wasira: Kazi aliyoifanya Rais Samia anastahili kuchaguliwa tena