September 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wasira: Kazi aliyoifanya Rais Samia anastahili kuchaguliwa tena

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema wakati wanamuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho, Dk. Samia Suluhu Hassan watanzania ni mashahidi kwa kazi kubwa aliyoifanya katika miaka minne na nusu ya uongozi wake. Anaripoti Zakia Nanga, Babati … (endelea).

Akizungumza tarehe 1 Septemba 2025, katika kikao cha ndani kilichohusisha viongozi na wana CCM Wilaya ya Babati, Wasira amesema kwa kuwa tangu Rais Samia amechukua uongozi kutoka kwa mtangulizi Hayati John Magufuli, kuna mambo makubwa yamefanyika nchini.

“Wanataka kumuondoa lakini sababu hawana na ukisema nao wapinzani pembeni wanasema lakini nyie wakubwa,mmefanya mambo mengi. Nilikuwa mjumbe wa kamati iliyoandika ilani mpya wa mwaka 2025-30 akanipigia kiongozi mmoja wa chama cha upinzani anasema nimeisoma ilami yenu mmeandika kila kitu sasa sisi tutaandika nini?

“Kwa sababu CCM tulikuwa na Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020 imetekelezwa mpaka tumevuka mpaka na ushahidi wake hata hapa Babati upo katika sekta zinazohusu watu. Tumejenga zahanati 19,vituo vya afya 8,tumejenga hospitali 2,moja ya kukarabati lakini kama imejengwa upya,” amesema Wasira.

Amesema, “Najua kuna tatizo la maji hapa lakini tumeikabidhi mamlaka ya maji ili kutatua changamoto hiyo. Kwa hiyo nakuja kuwaambia tumetekeleza Ilani na tunapokuja kuomba kura ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Watanzania ni mashahidi wa mambo makubwa yaliyofanyika katika kipindi cha miaka minne na nusu ya uongozi wake.”

Ameongeza wakati tunafikiwa miaka minne na nusu iliyopita kutokana na kifo cha Rais Hayati Dk.John Magufuli alimuachia Rais Dk. Samia kazi za kufanya alizozianzisha na wakati ule kulikuwa na hofu wanasema mwanamama huyu ataweza.

Amefafanua kwani wanaume wameshazoea mfumo dume mpaka Urais wanahusisha na mfumo dume utafikiri kila mwanaume anaweza kuwa tangu Rais.Hofu nyingine ilikua inajengwa tu na nyingine ni ya mazoea lakini Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kazi aliyoachiwa akaweka maneno mawili anakwambia KAZI IENDELEE.

About The Author

error: Content is protected !!