WATU 1000 wamepoteza maisha na mmoja kunusurika kutokana na maporomoko ya ardhi katika milima ya Marra, magharibi mwa Sudan, kutokana na mvua kubwa zilizonyesha katika mkoa wa Darfur. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kwa mujibu wa vikosi vya ukombozi wa Sudan (SLM/A),kijiji kilichoathirika kilikua makazi ya wakimbizi wa ndani waliokimbia mapigano ya Darfur Kaskazini kimezama kabisa ardhini.
Vinasema kuwa juhudi za uokoaji zinatatizwa na hali ngumu ya kijiografia na ukosefu wa vifaa.
SLM/A imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kutoa msaada wa haraka kwq manusura na kusaidia kutafuta miili ya waathirika.
ZINAZOFANANA
Umoja wa Afrika: Uchaguzi wa Tanzania ulivurugwa
Mambo matano makubwa kuhusu Raila
Raila Odinga alikuwa mwanaharakati wa demokrasia – Barack Obama