
ALIYEJIPACHIKA jina la mwanaharakati huru nchini, Cyprian Musiba, amejitosa katika mbio za ubunge katika jimbo la Mwibara, mkoani Mara, kupitia chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kabla ya kujiunga na ACT-Wazalendo, Musiba, alikuwa mmoja wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, walioshiriki mchakato wa kura za maoni katika jimbo hilo.
Kwa takribani miaka saba ya John Magufuli, Musiba alikuwa akijitambulisha kuwa mtetezi wa serikali na kutoa wito wa kuangamizwa wote wanaokwenda kinyume na mawazo ya Magufuli, hasa viongozi wa upinzani.
ZINAZOFANANA
Bulaya, matiko wapenya Kamati kuu CCM
ACT-Wazalendo wamjibu Polepole
Tutende haki, tutavuna amani