August 19, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Chadema yakwaa kisiki Mahakamani

Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema

 

MAHAKAMA Kuu masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ya kutaka kufunguliwa kifungo cha zuio la kufanya shughuli za kisiasa na kutumia mali zake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo wa shauri hilo la marejeo namba 14982/2025 umetolewa hii leo tarehe 18 Agosti 2025, mbele ya Jaji Hamidu Mwanga mara baada ya kusikiliza hoja kutoka pande zote mbili tarehe 7 Agosti mwaka huu.

Kufuatia uamuzi huo kesi ya msingi ya madai namba 8323 ya mwaka 2025, iliyofunguliwa na aliyekuwa makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar Said Issa Mohaamed na wajumbe wawili ya bodi ya wadhamini imepangwa kusikilizwa tarehe 28 Agosti Mwaka huu.

Kesi hiyo ilifunguliwa dhidi ya Bodi ya Wadhamini ya Chadema, wakidai kwamba Chama hicho, kimekuwa kikiitenga Zanzibar katika kuendesha shughuli zake ikiwemo suala la rasmali fedha.

Awali, wajumbe hao waliomba zuio la muda la chama hicho kutofanya shughuli zozote zile za kichama hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa, na tareje 10 Juni 2025, Mahakama iliwakubaliwa ombi hilo kwa kutoa zuio la muda kwa Chadema kutofanya shughuli za kichama.

About The Author

error: Content is protected !!