August 13, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kongwa kuchukua upya fomu za ubunge

Amos Makala, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kongwa, mkoani Dodoma, kimetangaza kuanza tena mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo hilo, kufuatia kufariki dunia kwa aliyekuwa mbunge wa hilo, Job Ndugai. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho, wilayani Kongwa, Julius Lepupuma, ameeleza kuwa zoezi hilo litafanyika kwa siku moja tu – tarehe 12 Agosti 2025, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Fomu za kuomba uteuzi, zitatolewa na katibu wa wilaya na katika ofisi za chama hicho wilayani Kongwa. Ndugai alifariki dunia tarehe 6 Agosti 2025.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa gharama za fomu zitaendelea kuwa kama zilivyoanishwa kwenye Kanuni za Uongozi katika vyombo vya dola, Toleo la 2025, huku ikisisitiza kuwa waombaji lazima wawe wanachama hai wa chama hicho, wenye akili timamu na waliolipia ada ya uanachama.

Aidha, chama hicho kimepiga marufuku maandamano au misafara ya magari, pikipiki, baiskeli, pamoja na matumizi ya ngoma au matarumbeta wakati wa uchukuaji wa fomu.

Vilevile, CCM kimekataza kuandaa wapambe kwa sherehe za kusindikiza wagombea.

About The Author

error: Content is protected !!