
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Magu, Joshua Nassari amemkabidhi rasmi ofisi Mkuu mpya wa Wilaya, Jubilate Lawuo kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Gabriel Mushi, Magu, Mwanza … (endelea).
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Nassari ameushukuru uongozi wa wilaya, watumishi wa serikali, taasisi binafsi na wananchi kwa ushirikiano mkubwa alioupata kipindi chote cha uongozi wake.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuendeleza miradi ya maendeleo na kuunga mkono juhudi za kiongozi mpya kwa maslahi ya taifa.
Kwa upande wake, DC Lawuo ameahidi kushirikiana na wadau wote wa maendeleo katika kuleta tija na ufanisi wa huduma kwa wananchi.
Makabidhiano ya ofisi yalifanyika jana Jumanne katika ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Magu na kuhudhuriwa na kamati ya ulinzi na usalama , mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Magu katibu wa CCM Magu na watumishi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya.
ZINAZOFANANA
Mohamed Abdulrahman: Gwiji la utangazaji DW laanguka
Msikubali pombe ikasababisha kurudisha nyuma maendeleo
Msiharibu miundombinu ya selikalini ili mjipatie kipato