July 12, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tundu Lissu akwama Mahakamani

 

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu, wa kuahirisha usikilizwaji wa kesi inayomkabili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa hii leo tarehe 11 Julai 2025, na Jaji Elizabeth Mkwizu, ambapo amesema kuwa maombi hayo yaliwahi kuwasilishwa mahakamani, walitakiwa kusubiri mpaka kesi ya msingi iishe ili kuangalia kama kulikuwa na hoja ya msingi, ndio wapeleke shauri hilo Mahakamani.

Maombi hayo ya Lissu yalikuwa yanahusu kesi yake ya tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao. Uamuzi huo wa kuahirisha kesi ulitolewa tarehe 2 Juni 2025.

Katika maombi yake, Lissu anaiomba Mahakama Kuu kuingilia kati na kufuta uamuzi huo wa Kisutu kwa madai kuwa umeathiri haki yake ya kusikilizwa kwa wakati.

About The Author

error: Content is protected !!