July 3, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Majaliwa autema ubunge Ruangwa

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania na mbunge wa Ruangwa

 

KASSIM Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mbunge wa Jimbo la ametangaza rasmi kutoagombea tena Ubunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruangwa … (endelea).

Majaliwa ambaye amekuwa mbunge katika jimbo hilo kwa takribani miaka 15 mfululizo tangu mwaka 2010.

Uamuzi huo umeutangaza leo tarehe 2 Julai 2025 na Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM)- Wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi Abbas Makwetta ambaye amesema ” Waziri Majaliwa amekuja na kusema hangobei tena ubunge”

Amesema amelitumikia jimbo kwa kipindi cha miaka 15 ametafakari na kuamua awaachie vijana ili waendelee na hatua zingine, lakini amewataka wana Ruangwa kuhakikisha Samia, Mwinyi wanapata kura za kutosha.

Akiwa jimboni kwake Ruangwa kwa siku kadhaa za mashauriano na wananchi na wazee wa eneo hilo, Majaliwa amefikia uamuzi huo baada ya tafakari ya kina na ushauri wa wadau mbalimbali na amewashukuru Wanaruangwa kwa kipindi chote cha miaka 15 ya kumpa ubunge na kuwawakilisha vyema.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya Majaliwa kutangaza Bungeni, 26 Juni 2025, kuwa anapanga kugombea tena ubunge wa jimbo hilo, akisisitiza kuwa anaendelea kuhitaji ridhaa ya wananchi. Hata hivyo, kauli hiyo sasa imebadilika rasmi.

“Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena.”, alinukuliwa bungeni.

Uamuzi wa Majaliwa umepokelewa kwa hisia tofauti, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa wakiutaja kuwa ni uamuzi wa busara na wa kiungwana, hasa baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka 10 cha Uwaziri Mkuu tangu alipoteuliwa mwaka 2015.

About The Author

error: Content is protected !!