June 16, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kesi ya Lissu shahidi wa kwanza wa Serikali aanza kutoa ushahidi wake

Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema akiwa mahakamani Kisutu

 

SHAHIDI wa kwanza wa Jamhuri aliyejitambulisha kama PF 22863 Inspekta Jonh (45) aliyekuwa Inspecta wa Polisi tangu tarehe 6 Juni 2025 na kwamba kabla ya hapo alikuwa Inspacta msaidia wa Jeshi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Shahihi huyo aliyesoma Chuo cha Polisi Zanzibar na 2005 na kumaliza 2006 na kutunikiwa cheti cha Competence.

Shahidi huyo aliyeongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga alidai kuwa anafanya kazi chini ya ofisi ya Mkurugenzi wa makosa ya jina katika kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandao (cyber crime investigation) Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam.

Shahidi huo alidai kuwa majukumu yake ni mpelelezi katika doria ya mtandaoni.

Inspecta John amedai mahakamani hapo kuwa anafanya doria kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo:- Facebook, Tiktok, YouTube, Instagram na mitandao mengine.

Shahidi huyo alidai kuwa YouTube ni mtandao wa kijamii unaowakutanisha watu pamoja ambao mtumiaji anapaswa kujisajili kulingana na vigezo vilivyowekwa na kwamba ukishajisalili mtumiaji anaweza kuchapisha picha mjongeo ambayo ni video vilevile unaweza kutoa maoni kwa video iliyochapishwa na mtumiaji mwingine au ku-like.

Shahidi huyo amedai kuwa Instagram ni mtandao wa kijamii ambao mtumiaji naye anapaswa kujisali kwa jina utakalopendekeza ili watumiaji wengine wakuone pia amedai kuwa kwenye mtandao huo unaweza kuchapisha picha au video au kuwa mfuatiliaji pia kutuma meseji ambayo haiko wazi kwa watumiaji wengine.

Shahidi huyo alipoulizwa wakati anaongozwa kutoa ushahidi wake juu ya vifaa anavyotumia kufanya doria amejibu kuwa wanatumia kompyuta maalum waliyopewa na ofisi ambayo ni mali ya Jeshi la Polisi.

Amedai kuwa doria anayofanya yeye ni kutembelea mitandao mbalimbali kwa ajili ya kubaini makosa mbalimbali yanayofanywa na watumiaji wa mitandao hiyo.

Shahidi huyo aliyesoma chuo cha Uniq Academy Upanga jijini Dar es Salaam alihudhuria mafunzo ya Computer Hacking kwa muda wa miezi miwili na kupata cheti.

Inspecta John amedai kuwa jukumu hilo amelianza 2020 mpaka sasa akiwa na uzoefu wa miaka minne.

Akiielezea umadhubuti wa kompyuta hiyo kuwa ni salama kwa kuwa zinanyilwa (password) na kuiupdate mara kwa mara.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online kwa muendelezo wa taarifa hii….

About The Author

error: Content is protected !!