
Juma Mrai, Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetoa wito kwa vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2025 kutoka shule zote Tanzania Bara, kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2025. Anaripoti Joyce Ndeki, Dodoma … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dodoma, Juma Mrai, Kaimu Mkuu wa Utawala wa JKT, amesema vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye kambi mbalimbali kuanzia tarehe 28 Mei hadi tarehe 8 Juni 2025.
Ametaja kambi ambazo wahitimu hao wa kidato cha sita watakwenda kuripoti kuwa ni JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvuma na JKT Kibiti – Pwani, JKT Mpwapwa na JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga -Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni na JKT Orjolo – Arusha, JKT Bulombora, JKT
Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma, JKT Itaka – Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa – Rukwa pamoja na JKT Nachingwea – Lindi.
Kanali Mrai ameongeza kuwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical Disabilities) watatakiwa kuripoti katika Kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa aina hiyo.
ZINAZOFANANA
Mradi wa PURE Growth Fund wafungua maombi na mapendekezo ya Nishati Safi na Biashara za Kilimo
Mpina ashangaa watu wanatekwa Waziri bado yupo ofisini
Mafanikio Makubwa ya Mkutano wa 37 wa ISGE na Kongamano la 28 la AGOTA