September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Ni Meridianbet tena ndani ya Kijitonyama

 

Meridianbet tena ndani ya Kijitonyama ndivyo unavyoweza kusema kwakua leo tena wamefanikiwa kufika kwenye eneo hilo na kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu mbili ambazo zinapatikana maeneo hayo.

Huu ni utamaduni ambao wameujenga Meridianbet kwa muda mrefu kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii, Hivo leo wameamua kurudisha kwenye jamii kwa kutoa msaada wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira kwa timu mbili za mpira wa miguu ambazo ni Magic Fc, pamoja na African Boys Fc.

Bashiri michezo mbalimbali ambayo imepewa ODDS BOMBA pale Meridianbet wikiendi hii Bila kusahau kucheza michezo ya Kasino uibuke mshinde wa Mamilioni

Mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wanatambua fika kua michezo imekua sehemu inayotoa ajira kwa vijana wengi haswa mpira wa miguu, Hivo wao kutoa msaada kwa timu hizo za mpira wa miguu imeonesha kua wanapambana kuhakikisha ajira zinapatikana kwa wingi kwa vijana kupitia michezo.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko kutoka Meridianbet Nancy Ingram alipata wasaa wa kuzungumza wakati wa tukio hilo “Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani kwa mapokezi mliyotupatia mahala hapa lakini kubwa ni kufanikisha hili ambalo tumelifanya hapa tuna matumaini tutapata wachezaji wazuri sana siku za mbeleni kupitia timu hizi”

Aidha viongozi wa timu za Magic Fc, pamoja na African Boys walifanikiwa kutoa shukrani zao za dhati kwa uongozi wa Meridianbet kwa msaada walioutoa kwao wakitoa wito kwa makampuni mengine kujitahidi kutoa misaada ili kuhakikisha wanaibua vipaji vipya kila siku.

About The Author