
Charles Ong’ondo Were
MBUNGE mmoja nchini Kenya ameuawa kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).
Charles Ong’ondo Were alikuwa ametoka bungeni muda mchache tu kabla ya kushambuliwa akiwa ndani ya gari lake kwenye barabara iiliyo na shughuli nyingi mjini Nairobi.
Polisi wamesema gari la mbunge huyo Charles Ong’ondo liliandamwa na watu wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki- kisha mmoja wao akasimama na kumfyatulia risasi kadhaa.
Dereva wake alinusurika shambulio hilo.
Marehemu ni mbunge wa chama cha mwanasiasa mkongwe Raila Odinga.
Polisi wangali wanachunguza kisa hicho huku waliotenda uhalifu huo wakiwa bado hawajakamatwa na nia ya mauaji hayo haikubainika mara moja.
Dereva wa gari na abiria wa kiume, ambao hawakujeruhiwa walifanikiwa kumkimbiza mbunge huyo katika Hospitali ya Nairobi, ambapo alitangazwa kuwa amefariki wakati anawasilishwa.
Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wa Polisi Muchiri Nyaga, alithibitisha kwamba mbunge huyo aliuawa kwa kupigwa risasi Jumatano jioni kando ya Barabara ya Ngong karibu na mzunguko wa chumba cha kuhifadhi maiti cha City na mtu aliyekuwa na bunduki.
“Asili ya uhalifu huu inaonekana kuwa alilengwa na ulipangwa,” msemaji wa polisi aliongezea.
Muchiri alisema makamanda wakuu wa polisi na wapelelezi walitembelea eneo hilo kuchunguza kilichotokea.
Huduma ya Polisi ililaani kitendo hicho cha ufyatuaji risasi na kukitaja kama “uhalifu mbaya na usio na maana” na kuhakikishia umma kwamba hakuna kitakachozuia uchunguzi.
ZINAZOFANANA
Kardinali Becciu ajiondoa kumchagua Papa mpya
Amnesty yakosoa hatua za Trump akitimiza siku 100 madarakani
Mume wa Marehemu mwimbaji wa Injili ahukumiwa kunyongwa