
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
RAIS wa Marekani Donald Trump amesema kwa sasa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anaonekana kuwa mtulivu na mwenye nia ya kutaka kufikia makubaliano ya amani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Kauli za Trump zimetolewa wakati Moscow na Kiev zikiendelea kushambuliana vikali kwa makombora na droni, huku Korea Kaskazini ikithibitisha kuwa imewatuma wanajeshi wake nchini Urusi kusaidia katika vita hivyo hasa katika ukombozi wa eneo la mpakani la Kursk.
Aidha Trump ameusifu mkutano wao siku ya Jumamosi mjini Vatican, huku akimtaka pia Rais wa Urusi Vladimir Putin kusitisha mashambulizi nchini Ukraine na kukaa kwenye meza ya majadiliano ili kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
ZINAZOFANANA
UN walia kuzorota haki za binadamu Burundi
Tetemeko laua 800 Afghanistan, Pakistan
Uingereza yafunga ubalozi wake Misri