May 25, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mahakama Kisutu yaombwa kutoa spika nje kwenye kesi ya Lissu

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa spika nje kwa ajili Watanzania watakaokosa nafasi kwenye chumba cha mahakama kwa sababu ya watu kujaa kwenye kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu Mwenyekiti wa Chadema, itakayotajwa kesho tarehe 24 Aprili 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Heche ameyasema hayo leo tarehe 23 Aprili 2025, akizungumza na waandishi wa habari , Makao Makuu ya Chadema Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Heche akiwakumbusha ameendelea kuwahimiza wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kesho katia mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo.

Heche amewataka Polisi kuwaacha wananchi wasikilize shauri hilo kwa kuwa ni haki yao kwa mujibu wa sheria “Polisi wasifanye fujo kwa mtu yoyote kwa sababu makusudi yetu ya kwenda kusikiliza kesi ya kiongozi wetu ni makusudi ya amani kwa sabau hii kesi ipo kwenye mahakama ya wazi”

“Kesi hii kubwa yenye maslahi ya umma kesi ambayo hukumu yake ni kunyongwa mpaka kufa kwa hiyo hatutaki ifanyike kizani , tunahitaji hii kesi iwe wazi kwa kila mtu vyombo vyetu vya dola vikae pemneni na tunaiomba mahakama itoe spika nje watanzania wapate nafasi ya kusikiliza watakao kosa nafasi wasikilize kinachoendelea ndani ya mahakama kwa sababu Lissu ni kiongozi mkubwa wa upinzani na huwezi kumshtaki kama unamshtaki mtu aliyeiba kuku”

“Hata Mandela alivyoshtakiwa hata Makaburu weupe waliruhusu watu weusi wasikilize kesi ya kiongozi wao haiwezekani viongozi weusi mwenzetu wakamate mtu kwa kesi ya kisiasa halafu wazue hata wanaopenda waje kusikiliza” alisema Heche.

Wakati huo huo Heche aliiomba Serikali kuiondoa kesi hiyo kwa kuwa kesi hiyo ni ya uongo “Lissu sio mhaini , huwezi kufanya uhaini kwa rai ambaye hajawahi kuwa Mwanajeshi hana kikundi chochote cha kijeshi anachokiongoza hawawezi kuithibitisha popote mwisho wa siku itakuwa kesi kama ya Freeman Mbowe cha ajabu chini ya utawala wa Rais Samia kwa miaka minne amejaribu kuwafungulia viongozi wa chama hichi kesi ambayo alijaribu kumfungulia kesi ya Ugaidi Mbowe na Lissu kwa miaka minne yake viongozi wa chama kikuu cha upinzani wanafunguliwa kesi ya uongo”alisema Heche.

Heche amesema kuwa Chama hicho kimeanza kuona dalili za vitisho ili kukwamisha ziara ya Operesheni No Reforms No Election lakini amesisitiza kuwa ziara hizo zitaendelea ambapo tarehe 3 Mei 2025 katika Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida (Kanda ya Kati), baadaye Kanda ya Magharibi.

About The Author

error: Content is protected !!