
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkunguni Kariakoo Jijini Dar es Salaam muda huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Heche amekamatwa na Polisi baada ya jeshi hilo hilo Wilaya ya Kariakoo kukiandikia barua ya chama hicho kuzuia mkutano huo.
Barua hiyo iliyowataka Chadema kutofanya mkutano huo uliopangwa kufanyika katika mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni kwa sababu ya shughuli za biashara zinazoendelea eneo hilo.
ZINAZOFANANA
Shamba la Pinda labadili mtazamo wa wanafunzi Aniny Nndumi
Mbezi juu yashikwa mkono na Meridianbet
Chadema: Tundu Lissu yupo gerezani Ukonga