April 15, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mchome amtaka Msajili kuharakisha majibu ya barua yake

Lembrus Mchome

 

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Wilaya ya Mwanga, Lembrus Mchome amemuomba Msajili wa Vyama vya Siasa kuharakisha muafaka wa malalamiko aliyowasilisha kuhusu Uchaguzi uliofanywa na Kamati kuu ya Chama chake. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 8 Aprili 2025, amesema jambo hilo lina maslahi makubwa ya Taifa pamoja na Chama husika.

Aidha, Mchome amesema mapema hivi leo amepokea nakala ya barua kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa ikimtaka Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema kutoa majibu ya hoja zake alizowasilisha kwa msajili ndani ya siku tatu.

“Nimeenda kwa msajili kwa sababu ninayemlalamikia ni sehemu ya maamuzi ya vikao vya chama ikiwa na maana, Katibu Mkuu kama leo mimi nikikata rufaa baraza kuu, yeye ndiye atakayeenda kuanda hicho kikao na kitaongozwa na Mwenyekiti na Chama ambae aliongoza kikao ambacho nakilalamikia cha tarehe 22 Januari ni Sawa sawa na kesi ya Ngedere umpe Nyani,” amefafanua Mchome.

Kufuatia picha mjongeo fupi za kikao cha kamati hiyo wa tarehe 22 Januari alizoonesha na mnukuu. Katibu Mkuu akisema ”akidi ya kikao hicho haitakuwa tena asilimia 75 kama inavyoitajika kama kikao kinahusu ajenda ya uchaguzi, kwa sababu hakuna agenda ya uchaguzi akidi ya kikao hiki ni simple.”

Kufuatia maelezo hayo Mchome amesema kuwa hakuna mahali popote ambapo Katibu Mkuu ameonesha kamati kuu imekaa ikahairisha ajenda ya uchaguzi wala baraza kuu kukubaliana kupitisha azimio la kuondoa ajenda hiyo, hivyo amesisitiza kuwa kikao hicho kilikuwa ni kikao cha uchaguzi.

Aidha, Mchome ameeleza makosa mengine yaliyojitokeza katika kikao hicho ni pamoja na Katibu mkuu kuruhusu kikao kuendelea akiwa hana idadi kamili ya wajumbe pamoja na saini zao pia uwepo wa baadhi ya watu katika kikao hicho ambao walipiga kura na sio wajumbe wa baraza kuu.

“Baada ya hoja hizo nilimuomba msajili mambo machache, moja kubatilisha baraza kuu la tarehe 22, pili viongozi wote nane waliopatikana siku hiyo waenguliwe au uteuzi wao ubatilishwe, tatu maamuzi yote yaliyofanywa na kamati kuu ya Chama chetu kwanzia tarehe 22 yabatilishwe kwasababu yalipitishwa na kamati ambayo haina wajumbe halali, nne msajili aitake ofisi ya katibu mkuu iitishe baraza kuu upya ambalo litakuwa na akidi ya asilimia 75,” amesema Mchome.

 

About The Author

error: Content is protected !!