
Julius Mwita, Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu wa Chadema
ALIYEKUWA Katibu wa Sekretarieti ya Kamati Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Julius Mwita, amesema chuki, ubinafsi, visasi, hasira, uchungu na vinyongo ambavyo vipo kwenye uongozi wa sasa wa CHADEMA ndio vilivomfanya aondolewe kwenye nafasi aliyokuwepo. Anaripoti. Apaikunda Mosha. Dar es salaam…(endelea).
Akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari leo alhamisi tarehe 03 Machi 2025, Mwita amtoa ufafanuzi kufuatia taarifa nyingi ambazo zinasambaa mtandaoni, zinazoonekana kama ndio chanzo cha kuenguliwa kwake.
Amesema moja ya taarifa ambazo zimetumika ni meseji ambazo zilitumiwa na chombo kimoja cha habari ambacho hakukitaja, zilizoeleza kwamba kuna kundi la watu linaloitwa G57 linalopinga msimamo wa Chadema juu ya suala la ‘No Reforms, No Election’ na wadau wakasema jambo hilo ni usaliti na uhaini hivyo watu hao wanatakiwa wafukuzwe uwanachama
Hata hivyo Mwita amesema hajaumizwa kwa kitendo cha kuenguliwa kwenye nafasi hiyo, kwasababu ndani ya kipindi cha miezi miwili ambacho ametumika katika nafasi aliyokuepo ameishi kama yatima.
“Kwa kipindi cha miezi miwili ambacho nimechotumika kama Katibu wa Sekretarieti tangu tarehe 21 Januari, mimi binafsi nilikuwa kama yatima, unaishi na watu ambao unaona kama hawakuamini, wanakuchukulia kama mtoto wa kambo, mtu ambae hufai kuwepo sehemu fulani, upo kwasababu labda umependelewa au kuna mtu anakubeba huna uwezo,” amesema Mwita.
Aliendelea “zilipotoka picha za mwita yupo kwenye kikao cha kamati kuu cha tarehe 10 Machi alitukanwa nchi nzima, huyu mtu anafanya nini kwenye kamati? huyu ni msaliti, nikajiuliza maswali mengi sana! ivi kwasababu tu Mwita alionekana kwenye uongozi wa Chama uliopita uliokuwa unaongozwa na Freeman Mbowe ndio nimekuwa mbaya kiasi hicho?”
Amesisitiza kuwa kufukuzwa kwake si kwasababu ya kupinga msimamo wa chama kama ilivoelezwa bali yapo mengi ambayo yamesemwa yakiwa hayana ushahidi na mojawapo ni suala la kuharibu chaguzi za chama ambazo zimewaingiza wengine madarakani.
Kwa mujibu wa Mwita ameeleza kuwa, yupo mtu mwingine ambaye atafukuzwa madarakani hivi karibuni kwa sababu ya chuki, amesema hatomtaja lakini yupo na hii wiki haitaisha mtasikia naye amefukuzwa, amesema pengine labda baada ya kusema kidogo watamspea kuonesha kwamba amesema uongo lakini hamalizi hii wiki.
“Hata sasa ivi tunavozungumza wapo wajumbe wa Kamati Kuu waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe wanashughulikiwa sawasawa kwenye kundi la Kamati Kuu la WhatsApp, wanatukana wanasemwa vibaya na hii ni Chuki tu, visasi, vinyongo, uchungu,” amesema Mwita.
ZINAZOFANANA
Nchimbi: Chadema wasilazimishwe kushiriki uchaguzi 2025
Waziri Tabia ajilipua
Heche: Bila kufanya mabadiliko hatuwezi kushinda Uchaguzi