
Rais wa Marekani, Donald Trump
RAIS wa Marekani Donald Trump amekataa kueleza iwapo uchumi wa Marekani unakabiliwa na mdororo wa kiuchumi au kupanda kwa bei za bidhaa. Anaripoti Apaikunda Mosha, Marekani … (endelea).
Akizungumza na Fox News kwenye matangazo ya mahojiano Jumapili lakini yaliyorekodiwa siku ya Alhamisi, Trump alijibu swali kuhusu mdororo wa uchumi.
“Sipendi kutabiri mambo kama hayo. Kuna kipindi cha mpito kwa sababu tunachofanya ni kikubwa. Tunarudisha utajiri Marekani. Hilo ni jambo kubwa. Inachukua muda kidogo, lakini nadhani inapaswa kuwa nzuri kwetu,” Trump.
Kutokana na utawala wake kukiuka vitisho vya ushuru dhidi ya baadhi ya washirika wake wa karibu wa kibiashara, Trump aliulizwa ikiwa anatarajia kushuka kwa uchumi mwaka huu, akasema kuna “kipindi cha mpito.
Naye Waziri wa Biashara, Howard Lutnick, alisisitiza hakutakuwa na msukosuko katika uchumi mkubwa zaidi duniani, huku akikiri kwamba bei ya baadhi ya bidhaa inaweza kupanda.
Mjadala huu umetokea baada ya wiki tete kwa masoko ya fedha ya Marekani wakati wawekezaji wakikabiliana na kutokuwa na uhakika kutoka kwa utawala wake wa U-turn juu ya baadhi ya sehemu muhimu za sera zake za biashara kali.
ZINAZOFANANA
Papa Francis atoa kauli yake ya kwanza, awashukuru wanaomuombea
Korea Kusini kuchangia USD Mil 104 maboresho ya Muhimbili
Waziri Chana afungua rasmi onyesha la wiki ya Ubunifu wa Italia