February 27, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dk. Slaa: Sasa nipo tayari kurudi Chadema

Dk. Wilibroad Slaa

 

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa amesema kuwa alikuwa mwanaharakati lakini sasa yupo tayari kurejea kwenye chama chake cha zamani cha Chadema. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo ameyasema muda mchache baada ya kuachiliwa huru na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akishitakiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo kwenye ukurasa wake katika mtandoa wa X.

Leo tarehe 27 Februari 2025. Wakili wa Serikali Mwandamizi Job Mrema aliwasilisha nia ya Mwendesha mashtaka wa Serikali (DPP), ya kutoendelea na shauri hilo.

Kifungu cha 91 (1) cha Mwenendo wa mashataka kinampa mamlaka DPP ya kuondosha shauri lolote mahakama isipokuwa tu yake yaliyofika hatua ya hukumu.

Dk. Slaa amerejeshewa uhuru wake saa sita mchana na kukamilisha taratibu za magereza saa saba na dakika 40 ambapo alitoka nje ya mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu.

Kauli ya kwanza ya Dk. Slaa alipozungumza na waandishi wa habari alieleza kufurahia kuwa huru lakini pia kufurahishwa na msimamo wa sasa wa Chadema wa ‘No Reform, No Election’.

“Sasa niko tayari kurejea Chadema mwanzo nilikuwa kama Mwanaharakati lakini sasa nitaingia Chadema,” alisema Dk. Slaa.

Dk. Slaa mpaka anachiliwa leo zimetimia takribani siku 48 za kusota mahabusu tangu alipokamatwa tarehe 10 Januari 2025.

About The Author

error: Content is protected !!