
Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi
WAKILI Ipilinga Panya amesema mawakili wanapitia changamoto na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu vyombo vya dola vimekuwa vikiingilia na kuwawekwa vizuizini bila hatia wakati wakitekeleza majukumu yao ya kisheria. Anaripoti Apaikunda Mosha. Lindi … (endelea).
Amezungumza haya tarehe 19 Februari 2025, kwenye uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, akimuwakilisha Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi.
Amesema pale mawakili wanapotetea haki za watu au wanapotoa elimu kwa wahanga na watu wenye uhitaji baadhi ya vyombo vya Dola hasa polisi wahamiaji, mamlaka ya udhibiti wa Dawa za kulevya na TAKUKURU vinawakamata na kuwaweka vizuizini pale wanapohisi kwamba mawakili wanaingilia kazi zao.
Ameiomba serikali kutoa tamko la katazo kwa vyombo hivyo vya dola pamoja na kuagiza pia uwajibishwaji kwa maofisa hao wa vyombo vya dola kwani wanafifisha jitihada na za utendaji kazi wa haki na pia kushindwa kufikia wananchi ili wenye uhitaji wa misaada mbalimbali ya kisheria na utetezi pale wanapokuwa na masuala yanayohusu mahakama na sheria.
Aidha, mbali na changamoto hizo amesema TLS kimefanikiwa kutoa msaada kwa wananchi wengi, kwa takwimu za mwaka 2024 chama hicho cha sheria kimeweza kufikia wananchi 7,300, na pia kutoa msaada kwa wananchi moja kwa moja 623 kwa kuwasaidia kufika mahakamani ili kupata haki yao za kisheria.
ZINAZOFANANA
Samia: Uhitaji wa kahawa duniani ni fursa kwa Afrika
SBL yazindua kampeni ya SMASHED kukabiliana na unywaji wa pombe chini ya umri
DAWASA wajitia kitanzi changamoto za maji Temeke