![](https://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2025/02/NEC_1045.jpg)
VIONGOZI kadhaa wa madhehebu ya kidini mkoani Singida, wametakiwa kuwaonyesha wananchi umuhimu wa kuchagua viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kutumikia taifa, kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwishoni mwa mwaka. Anaripoti Nathaniel Limu … (endelea).
Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Singida, Halima Omari Dendege, wakati akifungua kongamano la utoaji elimu kwa viongozi wa madhehebu ya kidini, wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Alisema, sote tunajua kuwa mwaka huu wa 2025, ni mwaka wa uchaguzi na kwamba uchaguzi ni mchakato muhimu katika mfumo wetu wa demokrasia.
Mkuu wa mkoa amesema, rushwa katika uchaguzi inasababisha madhara makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa taifa zima.
Aidha, Dendega ametaja baadhi ya madhara ya rushwa katika mchakato wa uchaguzi, ni pamoja kukosekana kwa maamuzi ya uhuru.
Anasema viongozi ambao wanachaguliwa kwa njia ya rushwa, mara nyingi hawana uwezo wa kuleta maendeleo kwa taifa.
Badala yake, wanatumia mali za umma kwa manufaa binafsi na hivyo kuzorotesha maendeleo.
Dendego amesisitiza zaidi kwamba vita dhidi ya rushwa, ni vita yetu sote. Hivyo tuna jukumu la kuelimisha na kuhamasisha jamii. Alisema, ili uchaguzi wa 2025 uwe huru, haki na wazi, ni sharti mapambano dhidi ya rushwa yanashamiri.
Amesema: “Tutakapofanikiwa katika hilo,tutakuwa tumelinda demokrasia yetu, tumeimarisha utawala bora na tumehakikisha kuwa, taifa letu, linaendelea kwa maendeleo endelevu.”
Mapema akizungumza katika kongamano hilo, Afisa wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Joseph John Kailaya, amesema kuna umuhimu kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo viongozi wa dini, ili kutokomeza kabisa dhambi hiyo.
Alisema, kupitia TAKUKURU-Rafiki, wataendelea kushirikiana na viongozi mbali mbali wakiwemo wa dini.
Alisema, “kundi kubwa linatambua kuwa rushwa, ni dhambi. Kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, kutakuwa na vitendo vingi vya rushwa. Tushirikiane kuvikabili.”
Mbali na viongozi wa madhehebu ya kidini, kongamano lilihudhuriwa na viongozi wa kimila, wazee maarufu, watu wenye mahitaji maalumu na asasi zisizo za kiserikali.
Kongamano lililenga kutoa elimu juu ya rushwa katika uchaguzi mkuu wa 2025. Kauli mbiu ya TAKUKURU, ni kuzuia rusha.
ZINAZOFANANA
Malalamiko ya Chadema yalishafanyiwa kazi na Kamati
CCM yamfukuza aliyepinga uteuzi wa Rais Samia kugombea
Wassira apiga marufuku Chadema kuwatumia vijana Mara