February 13, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Malalamiko ya Chadema yalishafanyiwa kazi na Kamati

 

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wassira amesema Kamati maalumu iliyotokana na vyama vya siasa ilishauri Katiba na mifumo yake itajadiliwa baada ya uchaguzi kufanyika ili kuwepo na haki kwa watanzania wote. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dar es Salaam … (endelea).

Amezungumza haya mapema leo tarehe 13 Februari 2025 hii akiwa nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam kufuatia malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kwamba hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi (No Reform, No Election).

Amesema kuwa Rais Samia alifanya mazungumo ya mfumo wa maridhiano chini ya 4R na katika vyama hivo CHADEMA haikuwepo walisema matatizo ya uchaguzi na baada ya mazungumzo hayo sheria tatu zilifikishwa Bungeni ili kufanyiwa mabadiliko.

Wassira amesema kufuatia malalamiko hayo, Rais Samia aliunda Tume ya Uchaguzi ikapendekeza kuleta mabadiliko yanayosemwa lazima yabadilishe sheria tatu amazo ni sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani, Sheria ya Tume ya uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa na Tume wawakilishi walitoa maoni yao na kukafanyika mabadiliko lakini hawakuridhika kwa sababu wanataka kuwepo na kile wanachokitaka jambo ambalo si sawa.

Aidha Wassira amesema kufuatia uchaguzi wa Serikali za mitaa kulikuwa na manung’uniko kwa sababu waliweka watu hafifu na kule ambako hawakuwepo watu walikwenda kupiga kura zao za ndio au hapana kwa kuwa hawakujiandaa na uchaguzi huo na kwa mantiki hiyo ukishindwa huwezi kuacha kulalamika.

About The Author

error: Content is protected !!