February 11, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dk. Mpango mgeni rasmi kikao kazi cha Serikali mtandao

Makamu wa Tanzania, Dk. Philip Mpango

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango amesema serikali ya awamu ya sita ina jukumu la kuhakikisha kuwa sayansi, teknolojia na ubunifu zinatumika kikamilifu. Anaripoti Apaikunda Mosha, Arusha … (endelea).

Amezungumza haya leo tarehe 11 Februari 2025 katika kikao kazi cha tano cha serikali mtandao jijini Arusha akieleza ambavyo Serikali imejizatiti kuwekeza katika sekta ya Habari na mawasiliano ili kuchochea maendeleo na kuhakikisha inaendeleza shughuli zake kidijitali.

Dk. Mpango amesema, Katika idara ya 102 (L) ya mwaka 2025 uwekezaji katika sekta ya Tehama umesisitizwa, hasa uendelezaji wa miundombinu ya Tehama, upanuzi wa mtandao wa internet, huduma ya simu za mkononi, ujenzi wa vituo vya kuhifadhi taarifa na uboreshaji wa huduma za serikali mtandao kwa kujenga mifumo ya kidijitali ili kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

“Dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025 na rasimu ya Dira ya Taifa ya 2050 zimeitambua Tehama kama nyenzo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ambapo sekta zote za uchumi zitaendeshwa kwa Teknolojia ya kisasa,” amesema.

Amesema kuwa Tanzania imekuwa ikifanya vizuri katika eneo hili kwa mujibu wa utafiti, pia mikakati malimbali imeandaliwa katika kutimiza dhamira hii ili kufikia malengo hayo ikiwa ni pamoja na Sera ya Taifa ya Tehama ambayo inasimamia na kuongoza maendeleo ya Tehama nchini, mkakati wa uchumi wa kidijitali na mkakati wa kitaifa wa serikali mtandao.

Aidha amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa Tehama na kada nyingine kwa kuwawekea mazingira wezeshi  ya ufundishaji katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu.

Hata hivyo ameitaka mikoa miwili ambayo haikutajwa kuhakikisha kuwa wanaingia E-Office wanajiunga na mtandao  ifikapo tarehe 30 June, mwaka huu.

About The Author

error: Content is protected !!