February 11, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

CCM yamfukuza aliyepinga uteuzi wa Rais Samia kugombea

SAMSUNG CAMERA PICTURES

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemfukuza uanachama kada wa chama hicho, Mchungaji Godfrey Malisa kuanzia leo Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk. Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa chama hicho mwaka 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 10, 2025 Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa.

Mwananchi ilipomtafuta Dk. Malisa kuhusiana na uamuzi huo, amesema kuwa hakupewa taarifa wala kushirikishwa.

About The Author

error: Content is protected !!