![](https://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2025/02/Sam-Nujoma-CGTN-Africa.jpg)
RAIS wa Namibia Namgolo Mbumba, ametangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha mpambania uhuru wa Namibia Rais wa kwanza wa nchi hiyo Sam Nujoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Jumapili Ofisi ya Rais Namibia ilitangaza Sam Nujoma amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 katika mji mkuu wa Windhoek, alikokuwa akipatiwa matibabu kwa muda wa wiki tatu zilizopita kutokana na ugonjwa ambao haukuweza kupona.
Nujoma alikuwa kiongozi katika vita ya takribani miongo mitatu ya kupigania uhuru wa Namibia, kutokea katika utawala wa Afrika Kusini yenye ubaguzi wa rangi.
Pia, Nujoma alisaidia kupatikana kwa uhuru wa Namibia mwaka 1990, huku akishinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwaka huo na aliongoza nchu hiyo mpaka mwaka 2005.
Mbumba aliongezea kwa kusema kuwa, “Baba yetu mwanzilishi aliishi maisha marefu na yenye matokeo muhimu ambapo alitumikia kwa njia ya kipekee wananchi wa nchi yake anayoipenda.’’
ZINAZOFANANA
Waziri Chana afungua rasmi onyesha la wiki ya Ubunifu wa Italia
CCM yamfukuza aliyepinga uteuzi wa Rais Samia kugombea
ACT-Wazalendo chaunda Kamati ya Ilani