WATANZANIA wametakiwa kuachana na viongozi wa kisiasa wenye fitna na wachonganishi  kwani wanaleta chuki na uhasama hata pale mazuri yanapofanyika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pemba … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla wakati akizungumza na wananchi na wanachama katika viwanja vya Umoja ni Nguvu Kusini Pemba ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mikoa sita Visiwani Zanzibar.

“Sisi CCM tutetembee kifua mbele kwani kazi ya kuwahudumia wananchi tunaifanya inavyotakiwa, wale wenzetu ni watu wa vituko, uongo, fitina na majungu ndo kazi yao, sisi tunajukumu na dhamana ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Nayasema haya kwa sababu wanakuja hapa wanasema mnajenga maghorofa wakati watu wanakufa na njaa na miradi yote sio maendeleo sasa ndo ujue kuna shida na anaetamka hayo ni mtu mzima ndo mana nasema kazi ni kusema uongo na vituko lakini hawo hawo viongozi ndugu zao wanasoma katika hayo maghorofa na wanapata huduma mbalimbali lakini hawazioni niseme muda wa kudanganyana umeisha pamoja majukumu walilojipa tuwaogope Viongozi fitina,” alisema Makala.

Mwenezi Makalla ameendelea kusema kuwa Dk. Samia Suluhu Hassan na Dk. Hussein Mwinyi hawana ubaguzi wowote kwenye suala la kuwaletea maendeleo lakini wenzetu kila kukicha wanaweka fitina na hili kazi kwenu Wazinzabar kwa ujumla wakataeni Viongozi hao na wanasiasa hao kwa kuwanyima kura wakati Uchaguzi utakapofika na tuchague chama cha mapinduzi ambacho ndo kina wajibu wa kuyaleta.