TUNDU Lissu ameshinda uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kura 513 sawa na asilimia 51.5 akimzidi Freeman Mbowe Mwenyekiti aliyemaliza muda wake kwa kura 31 ambapo amepata kura 482 sawa na asilimia 48.3. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Mgombea mwingine Odero Charles Odero amepata kura moja sawa na asilimia 0.1 .
John Heche amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)- Bara kwa kura 577 sawa na asilimia 57.
Mpinzani wake Ezekia Wenje amepata kura 372 sawa na asilimia 37.
Naye Mathayo Gekul amepata kura 49 sawa na asilimia 5.
Said Mzee Saidi, Makamu Mwenyekiti Zanzibar amepata kura za ndio 625 sawa na asilimia 89.
ZINAZOFANANA
Mbowe aagiza kuunda kamati ya kuponya makovu ya Kampeni
Lissu: Sijawahi kugombana na Mbowe
Mbowe afungua Mkutano Mkuu akilia na matusi