January 22, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Jumuiya ya Wazazi CCM yawapiga biti mavimba macho Urais CCM 2025

 

JUMUIYA ya wazazi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) imetoa rai kwa makada wote wa chama hicho kuwa mbio za kufikiria kuwania kiti cha Urais zimeisha fungwa rasm na kama kuna mwana CCM anayedhani hawezi kuishi bila kuwa rais ajiunge na vyama vingine au asasi mbalimbali. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 21Januari 2025 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa,Fadhili Maganya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Jumuiya hiyo Jijini Dodoma juu ya msimamo wa chama hiyo kuhusu uchukuaji wa fomu ya kugombea Urais pamoja na mgombea mwenza.

Maganya akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kimetoa uamuzi wa kumpitisha mgombea Urais na mgombea mwenza na kwa kufanya hivyo makada wote wa CCM hawatakiwi kufikiria au kutegemea kuchukua fomu kwa maana ya kuwania nafasi hiyo na kuongeza kuwa yoyote anayedhani hawezi kuisi bila kuwa raisi basi ajiunge katika vikundi mbalimbali na agombee urais ambao kimsingi utakuwa na erufi ndogo.

“Napenda kutoa rai kwa wanachama wao wa CCM,Makada wote kwa suala la kupitia CCM ukurasa wa kugombea urais umefungwa rasm na kama mtu hawezi kuishi bila urais atafute vyama vingine hata vya michezo au kwenye taasisi mbalimbali ili apate urais wa erufi ndogo tu” ameeleza Maganya.

Akizungumzia juu ya kutangaza mapema juu ya kumtangaza mgombea urais na makamu wake amesema kuwa CCM ni chama ambacho ni kiwazi na chenye kuweka mambo yake adharani mapema na kujitofautisha na vyama vingine vya siasa.

Akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari Maganya ameeleza kuwa anaupongeza mkutano mkuu maalumu wa CCM kwa kufanya maamuzi sahihi ya kuwapitisha wagombea urais na makamu wake 2025 pamoja na kumpitisha Makamu Mwenyekiti CCM Taifa ambaye ni mwanasiasa mkongwe Steven Wasira.

Amesema kuwa kitendo cha wajumbe wa CCM kufanya maamuzi hayo ni kuonesha ukomavu wa chama na kufanya maamuzi muhimu kwa ajili ya ukomavu wa chama Tawala nchini.

About The Author

error: Content is protected !!