January 20, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mwabukusi: Chadema tutawaadhibu, msipowasiliza wananchi

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema Bara

 

BONIFACE Mwabukusi, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amewaonya wajumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwamba wakichagua kwa ushabiki bila kusikiliza sauti za wananchi watawaadhibu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwabukusi ambaye alishawahi kuwa mwanachama wa Chadema amesema ili Chadema isalimike wajumbe wasikilize maoni ya wananchi ambapo wanamtaka Tundu Lissu.

“Ukimuuona kiongozi anadharau social media hafai kuongoza …Wananchi washatoa maelekezo wachagueni Lissu tuwaunge mkono na wamesema msiponchagua Lissu watawaadhibu,” amesema Mwabukusi.

Amesema kuwa hampingi Freeman Mbowe kwa sababu ya kipimo cha muda wa kukaa madarakani.

“Simpingi Mbowe kwa sababu amekaa muda mrefu, nampinga juu ya mambo ya msingi na falsafa na misingi yao ya uendeshaji chama, lakini namuunga mkono Lissu na Heche namna ya falsafa zao,” alisema Mwabukusi.

Amesema wananchi wataheshimu uamuzi wao lakini wakichagua vibaya wananchi watawaadhibu.

“Wananchi tutaheshimu uamuzi wao lakini wakifanya makosa wasitupangie namna tutakavyowaadhibu wakichagua tofauti na Lissu tutawaheshimu lakini nao wao wataheshimu maamuzi yetu tutaheshimiana,” alisema Mwabukusi.

About The Author

error: Content is protected !!