BAADA ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kumpitisha kwa kishindo Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, amempendekeza Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wake. Anaripoti Mwandishi wetu , Dodoma … (endelea).
Rais Samia jana tarehe 19 Januari, 2025 alipita kwa kishindo cha kura zote za wajumbe wa mkutano mkuu kura 1924 sawa na asilimia 100.
Rais baada ya ushindi huo alisema kuwa ameridhia ombi la Dk. Philip Mpango ambaye ndiye Makamu wa Rais wa sasa la kutaka kupumzika.
Rais Samia akishinda uchaguzi Mkuu kuwa Rais , Dk. Nchimbi atakuwa Makamu wa Rais.
ZINAZOFANANA
Mwabukusi: Chadema tutawaadhibu, msipowasiliza wananchi
Mbowe, Lissu wawagawa viongozi wa Kigoma
Kinana atoa neno baada ya kupatika mrithi wake