MUDA mchache baadaye Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Abdurahman Kinana kupata mrithi kwenye nafasi hiyo amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuwa imani ya Watanzania kutokana na sera na uongozi wake kubwa imara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Mrithi wa nafasi hiyo ni Stephen Wasira aliyepigiwa kura 1924 na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho ulioketi tarehe 18 na 19 Januari 2025 jijini Dodoma.
Kinana alisema CCM ni chama imara, kikubwa na kinaheshimiwa na Watanzania na kimepewa dhamana ya uongozi wa nchi na hana shaka hata kidogo kitaendelea kupewa dhamana hiyo kwa sababu kina sera na ilani nzuri na kuwajali na kuwasikiliza wananchi.
Alisema Mwenyekiti huyo alimpendekeza mara mbili kuwa Makamu ambayo ni Aprili 2021 na Desemba 2022 na kumshukuru kwa heshima aliyompa na ataendelea kuienzi maisha yake yote.
“Kama kuna sifa zozote ambazo nimezipata ndani ya chama si zangu ni za wana CCM wote kwa sababu chama chetu si chama cha viongozi ni chama cha wanachama. Bila msaada wa wana CCM bila uongozi na imani ya viongozi nisingeweza kutimiza wajibu wangu kama nilivyofanya. Nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu nilifanikiwa kwa kiwango fulani,”alisema.
Aliwaomba wana CCM kumuunga mkono Rais Samia na kwamba wanampenda wanamheshimu na watathamini kazi kubwa anayofanya ya kujituma na kujitolea na kutekeleza ilani.
“Sina shaka hata kidogo katika uchaguzi ujao wana CCM watakupendekeza na watanzania watakuchagua ili tuendelee kupata maendeleo makubwa zaidi, nimpongeze Rais Hussein Mwinyi kwa kazi anayoifanya Zanzibar amekuwa mbunifu wa miradi mbalimbali na anafanya kazi kwa ufanisi,”alisema.
Aliahidi kuwa alipoandikiwa barua na Rais ya kuendelea kushirikiana na wana CCM katika kufanya kazi ya chama, atatimiza ahadi hiyo.
“Nimpongeze Wasira kwa kuchaguliwa nimepata nafasi ya kufanya kazi na Wasira ndani ya chama ni mtu hodari, mchapakazi, mwadilifu na mzalendo kwa taifa lake. Nina hakika nafasi ya Makamu Mwenyekiti iko salama chini ya uongozi wa Wasira,” alisema.
ZINAZOFANANA
Mwabukusi: Chadema tutawaadhibu, msipowasiliza wananchi
Mbowe, Lissu wawagawa viongozi wa Kigoma
Rais Samia kwenda na Dk. Nchimbi 2025