January 17, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kesi ya Dk. Slaa, mawakili waminyana Mahakamani

 

UPANDE wa utetezi katika katika kesi inayomkabili Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa umewasilisha pingamizi lao dhidi ya shtaka linalomkabili katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 17 Januari 2025 upande wa utetezi uliongozwa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi akisaidiwa na Peter Madeleka na wenzake wanne mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki.

Madeleka amedai mahakamani hapo kuwa shtaka hilo halina uhalali kwa sababu upelelezi haujakamilika kama ambavyo kifungi cha sheria Na.131 (A) (1) ambacho kiulazimisha upande wa Jamhuri usifungue mashtaka mpaka pale utakapokamilisha upelelezi.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Tawabu Issa umedai kuwa shtaka la Dk. Slaa ni la kuchapisha taarifa za uongo na limemtweza Rais wa Jamhuri .

Upande huo umesema kuwa matumizi ya neno ‘shall’ mahakama ya Rufaa ilishatoa tafsiri ya matumizi ya neno shall kwenye shauri la Bahati Makeja dhidi ya Jamhuri kesi ya rufaa Na.118 ya 2006. Katika shauri hilo mahakama ilisema ‘the word shall is not mandatory’ that word shall means relative and it subjected 388 CPA. Kifungu namba 388 kinapunguza makali ya matakwa ya lazima ya ‘shall’ neno sio kila linapotumika linamaanisha linamatakwa ya lazima.

Naye Edson Kilatu wakili wa utetezi amedai kuwa msingi kuunda kwa sheria namba 131 (A) (1) kumetokana na matumizi mabaya ya sheria baada ya kuonekana watu wengi wanashtakiwa bila upelelezi kukamilika na kupelekea watu kufurika mahabusu ndipo serikali ikapeleka muswada wa kufanya marekebisho ya sheria na kukazaliwa kwa kifungu hicho.

Utata waibuka

Wakati wakili Madeleka anafanya rejoinder (kujibu hoja zilijibiwa kwenye hoja zake) amedai kuwa kuitetea hati ya mshtaka dhidi ya Dk. Slaa ni kazi ngumu na kwamba labda yawe maelekezo.

Wakili Tawabu alisimama na kuomba mahakama imuamuru Wakili Madeleka kutoa ufafanuzi wa neno maelekezo.

Wakili Madeleka akajibu kuwa yupo kwenye rejoinder amwache amalizie kisha mahakama iamue.

Ulinzi mkali

Dk. Slaa afikishwa katika mahakama hiyo akiwa chini ya ulinzi mkali wa Askari Magereza.

Kizimbani amezungukwa na askari wawili kulia na kushoto kwake huku wengine mwengine watatu wakiwa wamejitawanya kwenye chumba cha mahakama.

Endelea kuifuatilia MwanaHALISI

About The Author

error: Content is protected !!