MWANAHARAKATI Maria Sarungi raia wa Tanzania, ametekwa nyara nchini Kenya na watu wenye silaha kali na kutokomea nae kusiko julikana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kenya … (endelea).
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linasema kwamba mwanaharakati na mhariri wa kujitegemea kutoka Tanzania Maria Sarungi ametekwa nyara akiwa nchini Kenya.
Katika taarifa kupitia mtandao wa X, shirika hilo limesema kwamba Maria alitekwa na wanaume watatu waliokuwa na silaha na ambao walikuwa na gari nyeusi aina ya Noah.
Aidha limeongeza kuwa kisa hicho kimetokea mwendo wa saa tisa na robo mchana katika eneo la Chaka Place, mtaa wa Kilimani mjini Nairobi.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Irungu Houghton ameiambia BBC kuwa wako katika eneo la tukio wakijaribu kupata taarifa zaidi.
ZINAZOFANANA
NIDA kutoa vitambulisho laki 4, waboresha mfumo
Maria Sarungi apatikana akiwa hai
Serikali yasisitiza umuhimu wa mafunzo ya ufuatiliaji miradi yake