January 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wanawake wapata jukwaa la ukombozi

 

ULE usemi usemao ukimkomboa mwanamke umeikomboa jamii unakwenda kutimizwa na Shirika la Mwanamke Salama Tanzania (SWO) kwa kuwakutanisha wanawake wote nchini kwa lengo la kuwatetea na kuwakomboa kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Catherine John mkurugenzi wa SWO , leo tarehe 9 Januari 2025 amesema kuwa jukwaa hilo limeanzishwa ili kuwa daraja na mafanikio kwa wanawake nchini .

“Shirika lina jukumu la kuwapa wanawake elimu ya uchumi, ujasiliamali,biashara na elimu ya afya ya akili”
Catherine aliongeza kuwa baada ya kumaliza kazi ya utoaji elimu shirikika hilo litamtafutia mwanamke fursa za mitaji kwenye taasisi mbalimbali za fedha nchi kwa ajili ya uchumi wa mtu mmoja mmoja pia biashara za pamoja lengo ni kuwafikia wanawake wote wenye biashara na wale wasiokuwa na biashara” amesema Catherine.

Amesema kuwa shirika hilo litapambana na ukatili wa jinsia ili kuhakikisha mwanamke na mtoto anakuwa salama.

Catherine amesema kuwa Shirika hilo halijaacha nyuma ajenda ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

“Rais wetu amekuwa championi wa ulimwengu kwenye suala la nishati safi ya kupikia nasi tutakuwa mabalozi na wahamasishaji wa Nishati safi itakoyookoa mazingira yetu lakini na afya za wanawake”

Mkurugenzi Catherine ametoa wito kwa wanawake wote nchini kujiunga na jukwaa hilo ili kunufaika na fursa mbambali za kiuchumi na zile za kijamii zinazopatikana kwenye shirika hilo.

About The Author

error: Content is protected !!