CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitaja siku ya tarehe 21 Januari 2025 kuwa ndio siku ya Mkutano wake mkuu wa uchaguzi utakaomchagua Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 16 Desemba 2024 , John Mnyika, Katibu Mkuu wa chama hicho amesema kuwa Mkutano mkuu huo utafanyika jijini Dar es Salaam mara baada ya chama hicho kukamilisha chaguzi za mabara yote ya chama hicho.
Mnyika amesema kuwa uchaguzi wa kwanza utakuwa tarehe 13 Januari 2025 utakuwa mkutano mkuu Mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha) sambamba na uchaguzi wao na Mkutano wa Baraza la Wazee (Bazecha) huku tarehe 16 ukiwa uchaguzi na Mkutano Mkuu w Baraza la Wanawake (Bawacha).
Mnyika ametangaza gharama za fomu ya kugombea ” nafasi ya Mwenyekiti wa Chama taifa fomu itagharamiwa kiasi cha shilingi 1,500,000 huku makamu Mwenyekiti Bara na kule Zanzibar shilingi 750,000″.
Fomu ya mgombea uenyekiti wa mabara yote itagharamiwa kiasi cha shilingi 300000 huku makamu mwenyekiti wa bara na Zanzibar wa mabaraza hayo watalipa kiasi cha shilingi 150,000 .
ZINAZOFANANA
John Tendwa afariki dunia
Lwakatare amkimbia Prof. Lipumba CUF
Prof. Kitila: Lissu ameudanganya Umma, hatukupanga mapinduzi