November 28, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kesi 2 za kughushi nyaraka ya Dk. Hirsi kuendelea Desemba 12, 2024

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kuendelea kusikiliza kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Hospitali ya Salamaan Dk. Abdi Hirsi ya kughushi nyaraka za Bima ya afya ili kujinufaisha tarehe 12 Desemba 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Shauri hilo lilitarajiwa kusikilizwa leo limeahirishwa mpaka tarehe hiyo na Hakimu Mkazi Mkuu Rahim Mushi

Katika shauri hilo Dk. Hirsi anadaiwa kughushi nyaraka za bima ya afya ya Strategis kati ya mwaka 2016 na 2023.

Katika shauri hilo Serikali iliwakilishwa na Wakili wa Serikali Tumaini Mafuru huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Juma Nassoro.

Wakati huo huo katika mahakama hiyo Dk. Hirsi anakabiliwa na shauri namba 19187 la mwaka 2024 linalohusu kughushi nyaraka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Gwantwa Mwankuga nayo ina mashatka ya kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia tija kinyume cha sheria .

Shauri hilo lilikuwa hatua ya usikilizwaji ushahidi nalo limeahirishwa kutoka na mapitio ya jarada hivyo litaendelea tarehe 12 Desemba 2024.

About The Author