KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) Oganaisheni na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Issa Gavu ameelezea hatua kwa hatua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika Mkoa wa Geita pamoja na mikoa mingine nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na kuboresha Kituo Cha mabasi Geita kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaokwenda kupata huduma katika Kituo hicho hawapati kero wala usumbufu na tayari fedha Sh.bilioni 14 zimetengwa kwa ajili ya Kituo hicho.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara alipokuwa akizindua kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Gavu amesisitiza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi imejipanga kuboresha kituo cha mabasi ili wananchi wapate huduma na tayari utaratibu wa kutafuta zabuni ili kumpata mkandarasi imeanza na muda si mrefu mradi utaanza kutekelezwa.
“Lengo letu ni kutaka kuona jamii ya Watanzania kila mmoja katika huduma zake anapata huduma iliyosafi na salama bila usumbufu wowote.Katika maeneo ya Mji wa Geita yako maeneo yaliyokuwa hajakamilika katika uimarishaji wa barabara za lami hivyo Serikali ya CCM imetanga fedha kwa ajili ya kuanza mradi wa ujenzi wa kilometa 17 za lami katika Mji huu wa Geita
“Lengo ni kuimarisha miundombinu ya barabara za lami katika Mji wa Geita ili kuupandisha hadhi Mji wetu.Katika upande wa elimu tayari Serikali ya CCM imejenga takriban shule 180 katika Mkoa wa Geita na shule hizo ni mpya ziko za msingi na Sekondari .Ipo shule ya wasichana yenye thamani ya sh.bilioni tatu.
“Hii ni kuonesha Serikali inamjali mtoto wa kike katika umuhimu wa kupata elimu lazima tuendelee tuendelee na kutuamini kwamba mipango yetu ni kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa faifa ya jamii kwa watu wa kizazi cha leo na kesho,”amesema Gavu.
Ameongeza kuwa miradi hiyo ikitunzwa itakuwa na faida kubwa kwa jamii huku akielezea pia hatua ambazo Serikali imechukua katika kuboresha huduma za afya kwani imejenga hospitali kubwa yenye thamani ya Sh.bilioni 20 katika Mji wa Geita ili kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.
Pia amesema Serikali ya CCM imeendelea kujenga zahanati,vituo vya afya pamoja na hospitali katika Mkoa huo na Mikoa mbalimbali nchini,hivyo amewaomba wananchi kuendelea kuwapa imani hiyo na wataendelea kuboresha maisha ya wananchi ili kila mwananchi afurahie uwepo wa Serikali ya CCM.
Kuhusu huduma ya upatikanaji umeme,Gavu amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya umeme katika Mkoa wa Geita na mikoa mingine nchini na kusisitiza Chama Cha Mapinduzi kimedhamiria kuendelea kuboresha huduma muhimu katika Jamii ya Watanzania.
ZINAZOFANANA
Polisi wadai Chadema wamewapiga mawe
Mbowe, Sugu wakamatwa na Polisi mkoani Songwe
Upelelezi wakwamisha kesi ya Boni Yai