JESHI la Israel limefanya mashambulizi kadhaa ya anga dhidi ya Iran mapema Jumamosi, kujibu kile jeshi lake linakiita “miezi ya mfululizo wa mashambulizi ” kutoka Tehran na washirika wake. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa BBC. (endelea).
IDF – Jeshi la Ulinzi la Israel – linasema kuwa linafanya “mashambulizi mahususi dhidi ya malengo ya kijeshi” nchini Iran, ambayo inaishutumu kwa “kuishambulia Israel” tangu tarehe 7 Oktoba 2023.
Uthibitisho wa IDF wa kuishambulia Iran ulifuatia ripoti za awali za vyombo vya habari vya Iran kuhusu milipuko kadhaa ndani na karibu na mji mkuu, Tehran.
Inakuja baada ya Tehran kurusha takriban makombora 200 ya balistiki kuelekea Israel tarehe 1 Oktoba, katika kile nchi hiyo ilisema ni kulipiza kisasi mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas katika ardhi ya Iran mwezi Julai.
Msemaji wa jeshi la Israel, Daniel Hagari, alisema Israel ina “haki na wajibu” wa kujilinda na “uwezo wake wa kujihami na kushambulia” “umehamasishwa kikamilifu”.
Marekani, mojawapo ya washirika wa karibu wa Israel, ilisema shambulia la Jumamosi dhidi ya Iran ni “zoezi la kujilinda.
Mengine kuhusu shambulio hilo hadi sasa.
Israel imethibitisha kufanya “mashambulizi dhidi ya ngome za kijeshi nchini Iran.”
Haijabainika ni maeneo gani yaliyolengwa na kiwango cha uharibifu hakijulikani.
Hapo awali Marekani iliionya Israel kutoshambulia maeneo ya nyuklia na mafuta ambayo yanaweza kuzua mzozo mkubwa katika eneo hilo.
Mashambulizi hayo yanakuja baada ya Iran kurusha takribani makombora 200 ya balestiki dhidi ya Israel mapema mwezi huu. Israel ilikuwa imesema italipiza kisasi lakini haikueleza kwa undani ni lini itafanya hivyo.
Iran ilifanya mashambulizi dhidi ya Israel kama hatua ya kulipiza kisasi mauaji kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh, kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah na kamanda wa operesheni wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran Brigedia Generali Abbas Nilforoushan.
Kufikia sasa, vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimepuuza mashambulizi hayo, jambo ambalo wataalam wanasema, ni jibu la kawaida Iran baada ya matukio kama hayo. Lakini, wataalam wanaonya, hali inaweza kubadilika ikiwa ripoti za uharibifu mkubwa au vifo zitaibuka.
Milipuko pia imeripotiwa nchini Syria lakini Israel haijadai kuhusika na mashambulizi hayo.
Vikosi vya ulinzi wa anga vya Syria vilinasa makombora na kuyaangusha, kulingana na Reuters huku shirika la habari ya AFP, likinukuu vyombo vya habari vya serikali ya Syria.
Marekani haikuhusika katika shambulio hilo, kulingana na Pentagon. Ikulu ya White House iliitaja shambulio hilo kuwa “zoezi la kujilinda.”
Rais wa Marekani Joe Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris wamefahamishwa kuhusu shambulio hilo wanafuatilia matukio hayo.
ZINAZOFANANA
Ushindi wa Profesa Lipumba wapingwa
Ukraine wakiri kufanya mauaji ya Jenerali wa Urusi na msaidizi wake mjini Moscow
Sativa amlipia Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti Chadema