September 19, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

BAKWATA yataka serikali kuchunguza mauaji na utekaji

BARAZA Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA), limetoa wito kwa serikali kuanzisha uchunguzi huru kuhusiana na matukio ya utekaji nyara na mauaji ya raia, vitendo vinavyodaiwa kutekelezwa na vyombo vya dola. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).

Wito huo umejiri siku moja baada ya Baraza kuu la Maaskofu (TEC), kutoa wito kama huo.

Bakwata imesisitiza kuwa uchunguzi huo utabainisha wahusika wa visa hivyo katili na bila upendeleo.

Akitoa kauli hiyo katika baraza la Maulid, katibu mkuu wa baraza hilo, Nuhu Mruma amesema, “Serikali inapaswa kuchukua hatua za dharura ili kurejesha matumaini kwa raia.”

Katika siku za hivi karibuni, asasi za kiraia na wanasiasa hasa wa upinzani, wameshinikiza serikali kuanzisha uchunguzi huru kutokana na mfululizo wa ripoti za watu kutoweka, kutekwa au hata kuuawa.

Mapema mwezi huu, aliyekuwa Kada wa Chadema, Ali Kibao, alitekwa akiwa ndani ya basi na watu wasiojulikana na siku moja baadaye mwili wake ulipatikana umetupwa katika eneo la Ununioi jijini Dar es Salaam.

About The Author