April 3, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Milipuko yatikisa Bujumbura

Spread the love

 

MJI mkuu wa kibiashara nchini Burundi – Bujumbura, umekumbwa na milipuko jana Jumanne, tarehe 31 Machi 2026. Anaripoti Karenga Ramadhani, kutoka Bunjumbura … (endelea).

Kwa mujibu wa mashuhuda, mlipuko hiyo, iliyoshuhudiwa jioni ya Jumanne, mingi imesababishwa na milipuko ya silaha nzito nzito ikiwemo mizinga iliyosikika kutokea maeneo ya Musaga, kunakopatikana kambi nyingi za kijeshi.

Hali hiyo ilisababisha mtafaruku mkubwa na kuzusha hofu kwa baadhi ya raia wakiamini kuwa ni mashambulizi ya kigaidi, au vita na wengine kufikiria jaribio la mapinduzi ya kijeshi.

Hii ni kutokana na milipuko hiyo imetokea, wakati Rais wa Jamhuri, Jenerali Evariste Ndayishimiye, akiwa nje ya Burundi. Rais Ndayishime yuko mjini Bangui, nchini Afrika ya Kati, anakohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Faustin Archange Touadéra, anayeingia kwenye muhula wake wa tatu wa urais.

Hata hivyo, msemaji wa jeshi la Burundi, Brig. Jenerali Baratuza Gaspard, amekanusha uvumi huo akieleza kuwa milipuko hiyo imetokana na shoti ya umeme ndani ya ‘Base Militaire” ambayo ni moja ya kambi kubwa ya jeshi zilizopo Musaga, kusini mwa Bujumbura.

“Tunaomba raia kutulia hasa wanaoishi kandokando ya eneo hilo kama Musaga, Gasekebuye na Kanyosha kujizuwia kutoka nje na kuzurura bila sababu za msingi,” alieleza msemaji huyo wa jeshi.

Akizungumza kwa njia ya kuonya, afande huyo aliwaita wazagazaji wa taarifa za uchochezi kwa nia ya kuvuruga usalama, kwamba serikali haitasita kuwachukuliwa hatua.

Wapenzi wa soka nchini Burundi, ni miongoni mwa walioathrika na milipuko hiyo, kufuatia baadhi yao walikuwa wakirejea majumbani wakitokea uwanja wa taifa wa “Intwari” kuhudhuria mechi ya kombe la Mataifa ya Afrika “AFCON” kati ya Burundi na Chad.

Katika mchezo huo, timu ya taifa ya Burundi, maarufu kama Intamba iliibuka na ushindi wa wa 4-0. Katika mzunguko wa kwanza uliyofanyika Ndjamena wiki iliyopita, Burundi ilishinda pia kwa 4-0.

Kufuatia hali hiyo ya mtafaruku, Rais wa Chad, Mahamat Itno Deby alisema, alizungumza kwa simu na Jenerali “Neva” akimpa pole ya mkasa huo.

Aliongeza kuwa “maafisa wa Burundi na duru za usalama wamehakikisha kuwa wachezaji wa timu yetu ya taifa ‘Sao’ wote wamesalimika na wanalindwa vizuri.”

Kauli kama hizo zimetolewa pia na baadhi ya ofisi za kibalozi za kigeni zilizopo Bujumbura kama Ufaransa na Ubelgiji zikiomba raia wao kusalia majumbani na kujihadhari na matembezi yasiokuwa na umuhimu.

Hakuna taarifa yoyote rasmi iliyotolewa mpaka sasa, kuhusu hasara iliotokana na milipuko hiyo au idadi ya watu walioathitika zaidi ya picha na sanamu zilizonaswa kibinafsi wakati wa milipuko.

About The Author

error: Content is protected !!