March 25, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

William Lukuvi afariki Dunia

 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi, amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya serikali iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, imeeleza kuwa Lukuvi, amekutwa na mauti leo Jumatano, tarehe 25 Machi 2026, majira ya saa moja asubuhi.

Mbunge huyo wa Ismani, mkoani Iringa, amekutwa na mauti, katika hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma. Alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya shinikizo la moyo.

Wakati wa uhai wake, Lukuvi aliwahi kushika nafasi mbalimbali serikalini, ikiwamo Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu), mkuu wa mkoa na mshauri wa Rais, masuala ya siasa.

Amekuwa bungeni tangu mwaka 1995 na tangu wakati huo, hakuwahi kutoka.

Alikuwa akitambulika na wenzake, kuwa mmoja wa wabunge wa muda mrefu kuliko wote waliokuwamo kwenye chombo hicho cha kutunga sheria.

William Vangimembe Lukuvi (70), alizaliwa tarehe 15 Agosti 1955, huko Mapogoro, mkoani Iringa.

About The Author

error: Content is protected !!