Benjamin Netanyahu
JESHI la Iran (IRGC), limeapa kumfuatilia na kumuua waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Vyanzo vya taarifa vya serikali ya Iran, ikiwamo shirika la habari la nchi hiyo – Mehr News Agency – limeripoti kuwa IRGC litaendelea “kumfuatilia na kumuua Netanyahu,” ili kupiza kisasi kwa mauaji ya viongozi wake.
Aidha, jeshi hilo limedai kuwa limeharibu maeneo kadhaa ndani ya Israel pamoja na vituo vitatu vya kijeshi vya Marekani katika eneo hilo wakati wa wimbi lake la 52 la mashambulizi.
Wakati huo huo, watu 20 wamekamatwa katika mji wa Urmia nchini Iran, wakituhumiwa kutuma taarifa za maeneo ya kijeshi, polisi na usalama kwa Israel.
Kwa mujibu wa Tasnim News Agency, shirika la habari lenye uhusiano na IRGC, mitandao kadhaa ya watu wanaodaiwa kuwa mamluki wanaohusishwa na maafisa wa Israel imefungiwa.
Watu hao 20 walikamatwa kufuatia amri ya mahakama, kwa mujibu wa mwendesha mashtaka mkuu wa jimbo la West Azerbaijan.
Wakati hayo yakiendelea, takribani watu 108 wameropotiwa kupelekwa hospitali wakiwa na majeraha katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Israel, watu hao wamepelekwa hospitalini wakiwa na majeraha madogo, wawili wakiwa katika hali ya “wastani,” huku watu tisa wakiendelea kufanyiwa tathmini ya kitabibu.
Tangu kuanza kwa mzozo huo, wizara hiyo inasema jumla ya watu 3,195 wamepatiwa matibabu hospitalini kutokana na majeraha yao.
Kati yao, watu 81 bado wamelazwa hospitalini kufikia leo Jumapili. Wizara ya afya haijatoa taarifa kuhusu idadi ya vifo vilivyorekodiwa.
Picha mpya zilizochukuliwa asubuhi hii, zinaonyesha uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya usiku kucha katika mji wa Holon, uliopo kusini mwa Tel Aviv.
Katika picha hizo, gari moja linaonekana limepinduka, vifusi vimetapakaa eneo hilo, na kuna shimo kubwa katika upande wa jengo la makazi.
Huduma ya dharura ya Magen David Adom (MDA) imesema ilitoa huduma ya kwanza kwa watu wawili waliokuwa katika eneo hilo wakiwa na majeraha madogo.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 80 alitibiwa kutokana na vipande vya kioo vilivyomjeruhi, huku mwanamke wa miaka 80 akitibiwa kutokana na kuvuta hewa ya moshi.
MDA imesema baadhi ya watu pia walipatiwa matibabu kutokana na mshtuko.
ZINAZOFANANA
Mojtaba Khamenei yuko salama kiafya na anaongoza kikamilifu – Iran
Nani alifariki pamoja na Ali Khamenei?
Mahakama yaamuru Wakazi kumlipa Mil 100 Baba Levo