March 5, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mazishi ya kitaifa ya Ali Khamenei yaahirishwa

 

MAZISHI ya kitaifa ya Kiongozi Mkuu wa Kiroho wa Iran, Ali Khamenei, yaliyokuwa yamepangwa kuanza leo tarehe 4 Machi 2026, yameahirishwa kwa muda usiojulikana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Awali, mazishi hayo yalitangazwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo, huku maandalizi yakiripotiwa kuendelea katika miji mbalimbali ya Iran. Picha na video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha maandalizi ya umma na ulinzi ukiimarishwa kabla ya tukio hilo kubwa la kitaifa.

Hata hivyo, kuahirishwa kwa mazishi hayo kunakuja wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa tete kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya kijeshi kati ya Iran na Israel.

Leo Jumatano, Serikali ya Israel imetangaza kuanzisha kile ilichokiita “wimbi kubwa” la mashambulizi mapya dhidi ya Iran, huku mapigano kati ya mataifa hayo mawili yakiingia siku ya tano mfululizo.

Mvutano huo unaendelea kuzua hofu ya kupanuka kwa mzozo katika eneo zima la Mashariki ya Kati, wakati jumuiya ya kimataifa ikiendelea kutoa wito wa kujizuia na kutafuta suluhisho la kidiplomasia.

Kuahirishwa kwa mazishi ya Khamenei kunatazamwa kama hatua ya tahadhari katika mazingira ya usalama yasiyotabirika, huku macho ya dunia yakielekezwa Tehran na Tel Aviv kuona iwapo mzozo huo utaongezeka au kutafutiwa njia ya mazungumzo

About The Author

error: Content is protected !!