February 28, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kuna dalili za kiongozi mkuu wa Iran kuuawa

 

MAOFISA wa ngazi ya juu wa Israel wanasema, Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamanei, ameuawa kwa makombora. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizonukuliwa na Reuters, Khamenei ameuawa kufuatia mashambulizi yaliyofanyika kwenye ofisi yake.

Naye Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amezungumzia shambulizi dhidi ya eneo la Iran la kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ambalo anasema,

“Kuna dalili zinazoongezeka zinazoonyesha kuwa “dikteta huyu” “ameuawa.”

Katika hotuba yake, Netanyahu amewaambia Wairan kuwa mashambulizi hayo yatawasaidia “kujiondoa katika udhalimu” na kuongeza kuwa wana “fursa moja tu” ya kupindua utawala wa Iran.

Akiongea kwa hisia kali, Nendeni alisema, “Nendeni wa wingi mitaani mumalize kazi hii. Huu ni wakati wenu wa kuwa huru.”

Kwamba, “Huu ni wakati muafaka wa kuungana pamoja kwa ajili ya misheni ya kihistoria.”

Amemalizia hotuba yake kwa kuwataka raia wa Israeli kusikiliza ushauri wa usalama kutoka kwa Kamandi ya Nchi baada ya kupendekeza kwamba operesheni dhidi ya Iran itaendelea “kadiri itakavyohitajika.”

About The Author

error: Content is protected !!