Tundu Lissu akiwa mahakamani
SERIKALI yaibuka na taarifa ya kutaka kuwasilisha kwenye kesi nyongeza ya ushahidi katika ushahidi wa ACP Aman Mahamba, kwenye kesi Na.19605/2025 inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu linaoongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na Jaji James Karayamaha na Jaji Ferdinand Kiwonde.
Leo tarehe 23 Februari Wakili wa serikali Mkuu Nassoro Katuga aliwasilisha mahakamani hapo ombi la kuongoza ushahidi wa shahidi wao ACP Aman Mahamba.
Awali Wakili wa serikali Mkuu, Renatus Mkude, ameeleza mahakamani hapo kuwa shauri hilo lilipangwa kwa ajili ya kusikiliza ‘notice’ taarifa ya kuongeza mashahidi na ushahidi na sisi tuko tayari.
Lissu, anasimama na kudai kuwa amepinga notice tangu wiki iliyopita na kwamba mahakama isikilize pingamizi lake.
Wakili Katuga anasimama na kudai kuwa utaratibu wa kisheria unawataka waleta maombi (serikalli), kuiwasilisha ili yeye apinge kama ana hoja ya kupinga haya sio maombi.
Lissu anadai kuwa sheria haitambui hicho kinachoitwa notice taarifa “hakitambuliki kisheria”,.
Katuga anaeileza mahakama kuwa tarehe 18 Februari 2026, waliwasilisha taarifa kuongeza ushahidi hiyo kwa njia ya mtandao kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha CPA.
“Pamoja na notice ‘taarifa hiyo”, ushahidi huu haumleti shahidi mpya bali ni nyongeza ya ushahidi wa ACP, Amin Mahamba. Kwamba ushahidi huu haujakuwa committed Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu,”amedai Katuga.
Amedai kuwa Mahamba ni mmoja wa viongozi wa timu ya upelelezi wa kesi hiyo na kwamba walibaini kuwa wanahitaji kuongeza ushahidi wake.
Anasimama Lissu, anadai kuwa Katuga amekwenda nje maelekezo ya majaji kwa kulihitajika utangulizi tu.
Katuga anasimama tena “Waheshimiwa kwani hiyo introduction ‘utangulizi uko chini ya sheria gani? Sisi tunaintroduce kwa namna tunayoona,”?
Lissu: Asinifundishe Sheria, asijaribu kabisa kunifundisha Sheria, anaanzaje kufanya submission ya hiyo notice kabla uhalali wake haujaamuliwa.
Katuga: Waheshimiwa hakuna bingwa wa Sheria, mabingwa ni nyie tu Majaji.
Jaji Ndunguru: Tumesikiliza hoja zote hivyo vijembe vyenu msivilete. Sasa mshitakiwa alisema anapingamizi na tukasema upande wa mashitaka walete open statement ili Mahakama iamue.
“Mambo mengine ya kwamba imeambatana na nini na nini kipo wapi hayo sio mambo ya msingi, mshitakiwa endelea sasa, hawa upande wa mashitaka mmemaliza hapo,” anasema Jaji Ndunguru
Lissu: Nieleze mambo yafuatayo:-
1. Upande wa mashitaka unasema notice yao haileti shahidi mpya bali inaongezea ushahidi wa shahidi ambae ushahidi wake ulishatolewa kwenye committal.
2. Wamemtaja huyo shahidi kwa jina kabisa.
3. Wamesema wameleta viambatanisho vinavyotakiwa kwa mujibu wa kifungu cha 308(2) cha CPA.
Lissu: anaendelea “Sasa baada ya kusema haya twende kifungu kinavyosema cha 308, kinachotakiwa kuletwa ni jina la shahidi wa ziada, huyu ndio anaweza kutolewa notice.
“Wamesema wenyewe hawaleti shahidi mpya bali wanaongezea ushahidi wa shahidi aliyepo, sasa waheshimiwa majaji naomba niwaalike kwenye ukurasa wa 90 na 91 na 99 na 100 wa record ya committal proceedings na ukurasa wa 134 wa record ya mahakama hii ambapo upande wa mashitaka ulitaja majina ya mashahidi wao.
‘Huyo Amin Mahamba yupo na mimi maelezo yake ninayo hapa sasa waheshimiwa majaji hiyo notice inaingiaje mahakamani, ushahidi wake tayari upo mahakamani na notice inatakiwa iwe ya shahidi ambae maelezo yake hayakusomwa mahakamani” amedai Lissu.
Lissu ameongeza “Hii sio notice ya additional witness (taarifa ya nyongeza ya shahidi ) ni notice ya additional evidence (nyongeza ya ushahidi) ambayo haipo kisheria nimetafuta CPA yote hicho wanachosema hakipo,”.
“Jambo lingine ni kwamba wanaleta ushahidi wa mtu aliyefanya upelelezi wa matukio ya uchaguzi mkuu 2025 sasa majaji matukio ya tukio ya tarehe 29/10 mimi tayari niko mahabusu”
Lissu: Wamesema wenyewe kwa midomo yao hapa mahakamani. Niliwaambia wasibwabwaje sana. wakang’ang’ania kuanza kusema mambo ya tarehe 29 Oktoba ndio maana na mimi nasema hayo ya tarehe 29 mimi nilikuwa jela.
Lissu amedai mahakamani hapo kuwa kama mahakama hiyo itakubali kupokea ushahidi wa ziada itajifunga kwenye mambo ambayo itashindwa kuyashughulikia.
“Wanataka tuzungumze mambo ya Oktoba 29 mtakuwa mmefungulia balaa na isije ikawa shida. Mkifungua huo mlango tutaenda huko. Tutazungumzia mauaji ya kimbali na tutaulizana nani aliyeua watanzania. Hii kitu haina mashiko. Are they ready? Mimi niko tayari. Isiruhusiwe ikiruhusiwa niko tayari,”alihoji Lissu.
ZINAZOFANANA
Rasmi zama za Lipumba CUF zimekwisha, Mirambo ashika hatamu
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yaridhishwa na uzalishaji umeme
Aliyemkamata mhamasishaji vurugu Mbeya atoa ushahidi kesi ya Lissu