Spika Mussa Zungu
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, amewataka Watanzania kujivunia lugha yao ya Kiswahili na kuepuka kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kukashifu viongozi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Wito huo ameutoa kufuatia kusambaa kwa picha mjongeo kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha baadhi ya wabunge wakibabaika kuzungumza lugha ya Kiingereza wakati wa uchaguzi wa wabunge watakaowakilisha taasisi mbalimbali za kitaifa, kikanda na kimataifa.
Zungu amesema ni muhimu kwa wananchi kutambua thamani ya lugha ya kiswahili kama utambulisho wa taifa na chombo cha umoja wa Watanzania, badala ya kutumia matukio kama hayo kuwadhihaki au kuwashambulia wabunge kupitia mitandao.
Amesisitiza kuwa fahari ya lugha ya taifa inapaswa kulindwa na kuthaminiwa, huku akihimiza matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa kujenga na si kubomoa heshima ya viongozi na taasisi za nchi.
ZINAZOFANANA
Magufuli alibadilisha fikra za uongozi Tanzania – Dk. Nchimbi
Balozi Nchimbi kuongoza miaka mitano ya kifo cha Magufuli
Mahakama yaamuru Wakazi kumlipa Mil 100 Baba Levo